Siku ya leo nimeona vyema tujifunze kosa ambalo wengi tunalifanya na kujikuta tunapoteza ndoto zetu.
KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kutafuta kosa la kwanza ambalo limefanya wengi wetu tuwe sehemu tofauti na kusudi.Kosa la kwanza ambalo wengi tunafanya ni MAAMUZI YA KUCHAGUA RAFIKI. Ili kulielewa somo hili nmejaribu kugawa vipindi vya umri na uhusiano wa kufanya maamuzi ya RAFIKI.
Fatilia kama ifatavyo;
#MAISHA KATI YA MWAKA 1 HADI 17.
Katika umri huu hakuna tatizo sana, maana wengi katika umri huu huongozwa na malezi ya walezi wao, pia katika umri huu wengi huwa hawajui nini maana ya rafiki katika mafanikio yao, ingawa kulingana na mabadiliko ya mwili vijana wengi hujaribu mengi na wanao jaribu mabaya huwa karibu na rafiki wa aina hiyo.
Ila huwa ni rahisi kurekebisha makosa ya uchaguzi wa rafiki katika umri huu.
#MAISHA KATI YA UMRI WA MIAKA 18 -28 (KOSA LA 1)
Hapa ndipo kosa la kwanza huwa na asilimia nyingi za kugeuza njia yako, katika umri huu ukikosea kuchagua rafiki kuna uwezekano usijue utofauti wako, Umri huu ni hatari sana maana vijana wengi huwa kwenye mkusanyiko ya watu wenye malengo tofauti, kibaya zaidi ni kwamba. ......kuna uwezekano kati ya watu kumi, watu watatu tu ndo wana uwezo wa kuishi maisha yao halisi ikiwa watajichanganya na watu wenye malengo tofauti na wao. .....
Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu ambao hawapo sehemu sahihi katika uzee wao, ndoa zao na mafanikio yao walifanya kosa hilo katika umri huu.
Makosa yapo mengi, ila ukipatia kuchagua RAFIKI kuna uwezekano mkubwa wa kuijua njia yako na kupunguza idadi ya makosa.
#MAISHA KUANZIA UMRI WA MIAKA 30 NA KUENDELEA.
Kama upo kwenye umri huu na ulifanikiwa kuwa na uchaguzi mzuri wa MARAFIKI sio tatizo sana, ila kwa walio kosea huwa hali sio nzuri kwao..............Tatizo moja kwa walio kosea na wapo kwenye kundi hili ni IMANI walizojijengea. .....hili ni tatizo kwa sababu kwa imani hizo inakuwa ni ngumu kurudi kwenye njia zao sahihi (ingawa kwa umri huu huwa ni Kazi kidogo kurudi kwenye ndoto uliyopoteza ingawa kurudi inawezekana ).
RAFIKI sio jambo la kawaida kama wengi wanavyolichukulia, ni jambo la tofauti katika kukufikisha kwenye kusudi sahihi.
Swali la kujiuliza. ..."unafahamu utofauti ulionao? Rafiki yako anatambua kwa nini yupo hapo alipo? "
Kabla ya kufikia umri wa kutumia nguvu kurudi kwenye njia yako sahihi hakikisha unafanya tasmini ya maamuzi yako ya kuwa na rafiki wa aina hiyo. ....
Tuonane wiki ijayo
See you at the top
Scientist Saul kalivubha
(0652 134 707 )