Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha kwa lengo la kufikia ndoto zetu. ...Leo tuna somo mpya la madhara ya kutojiamini katika kufikia ndoto zetu. ..karibu.
kusudi la somo.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza jinsi gani hali ya kutojiamini inaweza kuzuia ndoto zako za mafanikio. .... Somo letu limelenga hasa sehemu ya .Maana ya kutojiamini. Ukielewa vizuri maana ya kutojiamini,utajitambua upo upande upi,na mafanikio kwako yapo kwa asilimia ngapi,nimejitahidi kufafanua maana ya kutojiamini na uhusiano wake kwenye mafanikio.....karibu.
MAANA YA KUTOJIAMINI.
Kunarafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa ukoo wao sio wa biashara hivyo hata akianzisha biashara hatafanikiwa. .je ni sahihi?
Mtu mwingine alisema .." Hata asome vipi hawezi kufaulu kwa ufaulu wa kiwango cha daraja A (grade A)"...umewahi kujiona ukiwa kwenye hali ya kushindwa? .....Nini maana ya KUTOJIAMINI..?
Kutojiamini ni hali ya mtu kujiona mwenye mapungufu, hali hiyo humfanya mtu huyo kuona watu wengine wana uwezo wa juu kuliko yeye. ........Nini maana yake? Tujaribu kuangalia ufafanuzi wa hali ya kutojiamini kupitia maelezohaya hapa chinI. ..
1.Wanasikolojia wana zungumzia hali ya kutojiamini kama vita anayokuwa nayo mtu dhidi ya watu wengine ambaoanaamini kuwa wana uwezo dhidi ya kile anachofanya /anachotaka kukifanya. ...Upo katika hali hiyo?
Kuwa katika vita na watu wasiotambua kama unapambana nao ndio chanzo cha mtu kupunguza kujiaminI. ..maana hali hiyo humfanya mtu ajione yupo upande wa kushindwa muda wote.
2. kutojiamini inaweza kuwa pia hali ambayo mtu anajiona mwenye kuhitaji sifa flani ili akubalike kwenye jamii. ....Hali hii humfanya mtu huyo kujiongezea sifa ya ziada ili akidhi hisia zake, ...hapa ndipo watu wasiojamini huanza kutumia nguvu kubwa kupamba sifa kivuli ili tu aondokane na hali ya kujiona mwenye mapungufu. ..je unaweza kuitunza sifa uliyojiongezea muda wote wa maisha?
3.Kutojiamini inaweza pia kuwa hali ya mtu kuamini zaidi matokeo ambayo yametokana na Kazi za watu wengine....kwa hiyo muda wote mtu asiyejiamini...anakuwa anaishi maisha ya watu wengine ambao mtu huyo anakuwa amewapa uwezo wa ushindi. .. hali hii humfanya mtu asiyejiamini asijaribu jambo lolote lile kwa kutumia mawazo yako. ....je unaweza kufikia ndoto zako kwa kuishi maisha yakutegemea juhudi za watu wengine?
.
Kutojiamini ni tatizo ambalo linatajwa kama chanzo kikubwa cha wivu ambao umepelekea mahusiano mengi ya mapenzi kufa,kama sio mapenzi kufa basi itamfanya mtu asiye jiamini kuwa mtumwa wa mapenzi.
Kutojiamini kwa ujumla ni hali ambayo ukiwa inayo itakufanya uwe unaishi maisha ya watu wengine,maana utakuwa unajiona mwenye mapungufu muda wote,.......unajua tatizo la kujiona mwenye mapungufu muda wote?..Tatizo lake kubwa ni kushindwa kujaribu,mana kulingana na mapungufu unayohisi ni mengi kwako ,utajenga imani ya kukosea kwa kila jambo linalokuhitaji kujaribu,na kumbuka tu ni ngumu kufanikiwa kama una hofu ya kujaribu.
....
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134707.
Karibu kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu.
Friday, 5 May 2017
Wednesday, 26 April 2017
KUANGUKA KWA MTU ALIYEFANIKIWA
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa Mungu anaendelea kukupigania. ...karibu tujifunze.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze somo la kuanguka kwa mtu aliyefanikiwa, unaweza kuhisi tofauti kidogo kwa kuona somo hili kwenye blog hii. ..ila ni hali ambayo wewe pia unaweza kuwa shahidi kwa kuona baadhi ya watu wakipoteza mafanikio yao makubwa....kwa hiyo nataka tuangalie baadhi ya sababu zinazofanya watu wapoteze mafanikio yao, kwa kujua sababu hizo itakuwa msaada kwetu kulinda mafanikio yetu.
Zipo sababu nyingi ila leo nataka tuangalie sababu kuu tatu......karibu.
SABABU ZA KUANGUKA KWA MTU ALIYEFANIKIWA.
1.Marafiki wapya;siku zote mtu aliyefanikiwa huwa anakuwa
tofauti na wengine, mafanikio yake yanavuta watu wengi kuwa karibu yake, watu hao ni pamoja na wale ambao waliona kuwa hawezi kipindi alipoanza safari ya mafanikio. .....hiki ni kipindi kigumu sana kwa mtu aliyefanikiwa, ni kipindi kigumu kwake kwa sababu ya ugumu wa kutambua nani rafiki wa kweli kwake, .... mafanikio yake hupotea pale atapoanza kushirikiana na rafiki wanaoshangalia mafanikio yake na kusahau rafiki waliomfaraji kwenye shida. ..siku zote rafiki anayeshagalia mafanikio yako huwa sio rafiki mzuri, maana kufata mafanikio yako na sio uhalisia wako

2.Kulewa sifa; sifa ni sehemu ya lazima kwamafanikio yako. .tatizo sio kusifiwa, tatizo ni kuzitawala hisia za furaha itokanayo na sifa. ....Wanasikolojia tunaamini kuwa tabia nyingi zitokanazo na sifa huwa ni za uharibifu na majivuno. ..mtu aliyefanikiwa akianza kuziishi tabia zitokanazo na kusifiwa anakuwa kwenye wakati mgumu sana wa kusahau alipotoka na kubadili njia ya kumpeleka aendapo. ...hatari yake ni kupoteza mafanikio yake.
3.Kukosa maandalizi kabla; Kuna watu wanafanikiwa bila kujiandaa kuyaishi maisha ya mafanikio, ..maisha ya mafanikio yana changamoto zake, mtu aliyefanikiwa kuipitia. .lazima watu wasifie tena kubwa sana. ..ni muhimu mtu ukafahamu wapi unaelekea, na nini utakibeba, kutambua hilo itakusaidia kuwa makini na mambo ambayo yapo nje ya kuendeza mafanikio yako. ..kinyume chake ni kupoteza mafanikio.
Kufikia ndoto zako sio kushinda, ushindi ni kuendeza mafanikio yako. ..
Tukutane wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134707.
Friday, 21 April 2017
SIRI ZA UVUMILIVU -3
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ...nashukuru Mungu kwa uzima wangu na wako pia. Karibu kwenye sehemu hii ya tatu na mwisho wa somo letu la siri za uvumilivu....karibu tuendelee.
KUSUDI LA SOMO.
lengo la somo letu hili ni kujifunza siri zilizopo kwenye uvumilivu, na somo letu lina sehemu tatu. 1.maana ya uvumilivu. 2. faida za uvumilivu. 3.hasara za kukosa uvumilivu. ..Leo nataka tujifunze hasara zipi zinaweza kutokana na ukosefu wa uvumilivu. ...Kabla ya kuendelea ingia Google search na kuandika kalivubha blog siri za uvumilivu. ..hiyo itakusaidia kuendana na sehemu hii ya mwisho.

3.HASARA ZA KUKOSA UVUMILIVU .
Mambo karibia yote yenye matokeo mazuri yanahitaji uvumilivu ili kuweza kufanikiwa kupata matokeo hayo mazuri. .....nataka tujifunze hasara za uvumilivu kwenye sehemu hizi tatu. .mahusiano ,biashara na mafanikio kwa ujumla. .....karibu tuendelee.
MAHUSIANO; Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia kuwa anahisi kuwa anabahati mbaya, kwani huwa hadumu kwenye mahusiano. ..utafiti unadhibitisha kuwa watu wengi wameacha watu sahihi sababu tu ya kukosa uvumilivu, ..Mahusiano yana changamoto zake, na hii hutokana na mahusiano kuhusisha watu wenye asili tofauti....kumbe kuna mazingira yatahitaji uvumilivu dhidi ya madhaifu, uvumilivu dhidi ya mabadiliko ya hisia ambayo yanaweza kuwa chanzo cha maamuzi mabovu.
BIASHARA. Kosa ambalo wengi tunalifanya kwenye biashara ni kutengeneza imani ya kupata mafanikio ya haraka. ...Hili ni kosa kwa sababu biashara karibu zote zinahitaji muda wa kutosha ili kutoa faida kamili, huo muda wa kutosha unahitaji mtu mvumilivu, ...pia kwenye biashara kuna hasara, na mara nyingine kuna kuanza upya, yote hayo yanahitaji uvumilivu wa kutosha. .ukikosa uvumilivu ni ngumu kufanikiwa katika biashara...
MAFANIKIO KWA UJUMLA; kufanikiwa kwa ujumla ni kuwa kwenye hatua ambayo ni matokeo ya kushinda maumivu ya UVUMILIVU. ...Msanii wa filamu maarufu kwa jina la Sylivester Stalone Rambo aliwahi kusema alijaribu zaidi ya mara 70 na kushindwa mara zote, ila kilicho msaidia ni uvumilivu wake, hadi sasa ni muigizaji maarufu dunianI. inahitaji uvumilivu wa hali ya juu katika safari yetu ya KUFIKIA NDOTO ZETU. ...Ukikosa uvumilivu ni ngumu kufanikiwa kwa jambo lolote lile. ....jiulize ni maamuzi gani uliyafanya kwa kukosa uvumilivu?

Karibu wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha
0652 134707.
Wednesday, 12 April 2017
SIRI ZA UVUMILIVU -2
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni imani yangu kuwa Mungu katimiza mapenzi yake kwetu sote. ......
KUSUDI LA SOMO
.
Lengo la somo letu la leo ni kuendelea na sehemu ya pili ya siri za uvumilivu,Kumbuka tu somo letu lina sehemu tatu. 1.maana ya uvumilivu. 2.faida za uvumilivu. 3.hasara za kukosa uvumilivu.
Ni vizuri kama utafatilia sehemu ya kwanza kwa kuingia Google search na kuandika kalivubha blog siri za uvumilivu utaletewa sehemu hiyo. ....karibu tuendelee.
2.FAIDA ZA UVUMILIVU.
Kwenye maisha tunayoishi kuna hali kuu mbili zinazochanganya watu wengi sana katika kufanya maamuzi, hali hizo ni kupata kitu kwa wakati na kupata kitu nje ya wakati .Ili kuweza kuzitawala hali zote hizo mbili bila kufanya maamuzi hatarishi inahitaji uvumilivu. Nmejaribu kuelezea faida za uvumilivu kupitia hali zifatazo.
1.Kukwepa hasara, katika mazingira tunayopitia kuelekea ndoto zetu kuna faida na hasara tuzipatazo kama matokeo ya yale tufanyayo. .....zipo hasara zinakuja kama changamoto, ila zipo hasara huja kama matokeo ya kupoteza uvumilivu, .......mara nyingi mtu akishindwa kutawala hisia zake kwenye mazingira yasiyo ya kawaida hujikuta amefanya maamuzi yasiyo ya kawaida ambayo ni HASARA.
2.Kujiongezea thamani ; Wanasikolojia tuna amini kuwa mtu mwenye uvumilivu huwa ana tabia ya kunyamaza pia kwenye mazingira yenye kuhitaji uvumilivu, hii huongeza thamani ya mtu huyo kwenye jamii, maana anakuwa amefanikisha kuzitawala hisia zako ambazo zingepelekea matokeo mabovu kulingana na maamuzi yenye kukosa uvumilivu. ....
3.Kutimiza ndoto; kila mtu mwenye kujitambua lazima awe na ndoto za maisha, ....ila taarifa isiyo pendeza masikioni kwa wengi ni kwamba. ili kufanikisha ndoto zako huwa inahitaji muda mrefu kidogo. ....taarifa hiyo sio nzuri kwa wengi maana watu wengi hupenda njia za mkato ktk kuelekea ndoto zao, ila kwa kuwa swala la kufikia ndoto zetu linahitajI muda wale wavumilivu tu ndo wamekuwa wakifikia ndoto zao.
Kumbuka kuwa uvumilivu sio Kazi rahisi, lazima uumie, ila ukiweza kubeba maumivu ya UVUMILIVU , kuna uwezekano ukaziishi ndoto zako.
karibu tena katika sehemu ya tatu na ya mwisho wiki ijayo.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652 134 707 )

Friday, 7 April 2017
SIRI ZA UVUMILIVU -1.
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania, ...karibu.
Leo nataka tujifunze somo la uvumilivu kwenye harakati zetu za kuelekea ndoto zetu.
Kuliishi neno uvumilivu ni zoezi ngumu, ila matokeo ya kutoliishi neno hilo ni wengi wetu kupoteza ndoto zao. .lazima tuwe wavumilivu ili tuweze KUFIKIA NDOTO ZETU. ......jiulize swali hilI, Utabadilisha maamuzi mangapi? ..maana matokeo ya kukosa uvumilivu ni kubadili mawazo.
Tukutane wiki ijayo katika sehemu ya pili.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134 707.
Leo nataka tujifunze somo la uvumilivu kwenye harakati zetu za kuelekea ndoto zetu.
KUSUDI LA SOMO.
somo letu la siri za uvumilivu limelenga kufundisha sehemu zifatazo. 1.maana ya uvumilivu. 2. faida za uvumilivu. 2.Hasara za kukosa uvumilivu. ..karibu kwenye sehemu ya kwanza ya somo hili.1.MAANA YA UVUMILIVU.
Kuna watu ambao wana tumia neno uvumilivu ila hawajui maana yake, kuna watu wengine wanajua maana yake ila wanashindwa kuliishi neno uvumilivu hasa pale wanapokutana na mazingira yenye kuhitaji uvumilivu. nimetumia mifano kulifafanua neno uvumilivu, karibu tujifunze.- Uvumilivuni ni uwezo wa kutawala hisia zako kipindi unapopata matokeo tofauti na makusudio yako, Wanasikolojia wanazunguwa kuwa moja ya zoezi gumu ni kutawala hisia zako kipindi unapopata matokeo tofauti na makusudio yako. .....hii inasababishwa na tabia ya binadam kupenda kila kitu kifanyike ndani ya uhitaji wake. ....ila kuna mazingira ambayo lazima uweke uvumilivu , ....sio kila kitu utakipata ndani ya muda unaohitaji wewe, ukiweza kutawala hisia zako kipindi hicho utakuwa umeliishi neno uvumilivu.
- .Uvumilivu ni uwezo wa kutawala hisia zako kipindi watu (rafiki zetu ) wanaposhindwa kutufanyia kama tunavyohitaji. ....maamuzi ambayo wengi tumefanya hasa pale rafiki zetu wanapofanya tofauti na tutakavyo huwa ni maamuzi yaliyokosa uvumilivu, ni maamuzi ya kubadili (badala ya maamuzi ya kusubiri wakati mwingine )......uwezo wa kutawala hisia zako ndani ya mazingira hayo ni tafasiri ya kuliishi neno uvumilivu. .
- .Uvumilivu ni UPENDO, kipimo cha Upendo kipo kwenye uvumilivu, ukiona umeshindwa kufanya uvumilivu wajambo flani kuna uwezekano mkubwa kuwa huna Upendo wa dhati na jambo hilo linalohitaji kuvumiliwa...
Kuliishi neno uvumilivu ni zoezi ngumu, ila matokeo ya kutoliishi neno hilo ni wengi wetu kupoteza ndoto zao. .lazima tuwe wavumilivu ili tuweze KUFIKIA NDOTO ZETU. ......jiulize swali hilI, Utabadilisha maamuzi mangapi? ..maana matokeo ya kukosa uvumilivu ni kubadili mawazo.
Tukutane wiki ijayo katika sehemu ya pili.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
0652 134 707.
Thursday, 30 March 2017
HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha, ni siku nyingine Mungu amefanya tukutane kwa lengo la kufundishana jinsi ya kufikia ndoto zetu
.
KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze machache kuhusu hatua ya awali katika safari ya maisha yenye ushindi, bado kuna watu ambao wamejaribu kila namna ya kupiga hatua ili kufikia malengo yao ila badala ya kusogea mbele wao wanarudi nyuma. ........Kibaya zaidi watu hao wameshindwa kufanya tasmini ya matokeo yao ambayo hayaridhishi. ..
Tatizo nini? .....zinaweza kuwa zipo sababu nyingi ila sababu kubwa inaweza kuwa ni kosa la awali. ...ni lipi hilo? .....karibu tujifunze.
HATUA YA KWANZA KWENYE MAFANIKIO.
Unapoweka malengo ya safari yako lazima ujue mambo muhimu ya kukufanya upige hatua, bila hivyo unaweza kuwa na malengo mazuri yasiyo tembea, zipo njia nyingi ambazo watu tofauti tofauti wanaweza kuzieleza, ila kwa upande wangu taeleza njia tatu za kufanya uweze kupiga hatua, njia ambazo hutengeneza hatua ya awali na muhimu kwenye mafanikio yako. .....njia hizo ni hizi ;
1.Kuwa na marafiki sahihi.ni usemi wa kila siku kuwa mafanikio yako yapo kwa rafiki yako, ila wengi huwa hatujui hilo, bora utumie muda mrefu kuishi bila rafiki kuliko kuwa na rafiki asiyetambua umuhimu wa kusudi lako,Watu wengi wameshindwa kufika waendapo kwa kuwa karibu na marafiki hasi, ....lazima uwe na rafiki sahihi ili uweze kupiga hatua
.
2.Matumizi ya muda. Kwenye matumizi ya muda ndipo kuna mafanikio yote (tembelea Google search uandike muda wa ziada kalivubha blog ujifunze matumizi sahihi ya muda).Ni ngumu kupiga hatua yoyote ya mafanikio ikiwa bado una matumizi mabovu ya muda, kuna mambo ambayo lazima uyafanye ili yakupe kibali cha kuendelea, mambo hayo yanahitaji uwe na matumizi mazuri ya muda wako, hatua ya awali ni pamoja na kuwa na ratiba zinazofata muda wako vizuri.
3.Kutambua madhaifu yako. ..wanafalsafa wamewahi kuzungumza kuwa, .."mtu anaekushinda mafanikio kuna mambo anayofanya ambayo wewe hufanyi "..nini maana yake?.ni muhimu kufanya tasmini ya madhaifu ambayo yanaweza kuwa sababu ya kuzuia hatua zako, hiyo itakusaidia kujifunza namna ya kupiga hatua kwa kutumia njia tofauti tofauti zenye kuziba madhaifu yako, ..kujifunza kwa kupitia watu waliofanikiwa sio vibaya, lazima ujue nini ambacho wao wanakushinda .
Ni hatua chache sana za kukufanya upige hatua kwenye malengo yako, ila ni watu wachache sana wamekamilika katika hatua zote hizo tatu, ...fanya tasmini ya maisha yako.
See you at the top.
scientist Saul kalivubha.
(0652134707 )

Wednesday, 22 March 2017
MUDA WA ZIADA -2
Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha kila jumatano
jumatano ya wiki, nashukuru Mungu
kwa kuendelea kunisamamia....karibu.
tujifunze.
KUSUDILA SOMO.
Kabla ya kuendelea na kusudi la somo letu hili, nikukumbushe kuwa somo letu lina sehemu mbili. 1.SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MUDA WA ZIADA.
2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.........
ili tuwe sambamba pitia somo la sehemu ya kwanza, tembelea Google search na kuandika kalivubha blog muda wa ziada au Tembelea page ya FIKIA NDOTO ZAKO Facebook.
Leo tunaendelea na sehemu yetu ya pili.
kumbuka kuwa muda wa ziada ni muda baada ya majukumu ya pamoja, huu ni ule muda ambao upo chini ya utawala wako katika matumizi. .....karibu tuendelee.
2. MATUMIZI MABOVU YA MUDA WA ZIADA.....
KUWA NA MAMBO MENGI;Kuwa na mambo ambayo yana positive effect (matokeo chanya)kwenye ndoto yako sio tatizo, tatizo ni pale mtu anapokosa utaratibu katika kupanga mambo yanayostahili kwanza yawe mbele. ..ukianza kutumia muda wako wa ziada leo kufanya mambo ya kesho hata kama ni mazuri, utakuwa unapoteza muda, ....lazima uwe na utaratibu katika kufanya mambo yako ili upate muda wa kutosha kufanya yanayostahili kwanza.
STAREHE; hapa ndipo kundi kubwa la watu lipo, maana wengi wanajua starehe lazima itumie pesa .........hata
ukitumia muda wa ziada kwa mambo yaliyo nje ya ndoto zako tunasema upo
kwenye starehe.
Hili tatizo wanalo watu wengi ambao hawana malengo, ambao hawaumii kutumia sentensi hiii. ."NIPO NAPOTEZA MUDA ".....kila muda unaopoteza lazima utaulipa , je utaulipaje? .....utaulipa kwa majuto.
KULIPA NAFASI JAMBO MOJA. ...hapa tuelewane vizuri , kuna watu ambao wapo addicted na jambo flani, muda wote wa ziada anakuwa busy na jambo hilo tu. .....sio tatizo ikiwa ndio maisha yako yapo kwenye jambo hilo, ..ila kama kuna mambo mengine yamebeba maisha yako ,utakuwa unapoteza muda kwa kufanya jambo hilo moja. ....toa nafasi kwa mambo mengine pia. ...
NB....Kila muda unaopoteza, lazima utaulipa kwa majuto yasiyo na tiba,wengi wetu huwa tunapuuzia usemi huo sababu madhara ya kulipa muda huo huwa yanachelewa. .ila
muda ukifika wa kulipa muda huo lazima mtu akumbuke mambo yaliyo poteza muda wake. .....
Tumia muda wako vizuri leo, ndoto zako zipo kwenye matumizi mazuri ya muda wako wa leo. .........
Unatumiaje muda wako wa ziada?
Karibu kwenye somo mpya muda kama huu. ....

Subscribe to:
Posts (Atom)