Tuesday, 24 October 2017

JITENGENEZEE KESHO YENYE MATUNDA.

Habari za kwako rafiki ambaye tumekuwa pamoja kwenye darasa hili la maisha ,kwa lengo la kusaidia kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa kuendelea kutupigania,karibu tujifunze.

Kusudi la somo.
Leo nataka tujifunze namna tunavyoweza kutengeneza kesho yetu iliyo ndani ya ndoto zetu,somo hili kwa bahati mbaya wengi wanalipata wakiwa tayari wamekosea sana kiasi kwamba kuanza safari upya inakuwa ngumu ,hivyo wanaamua kuendelea na safari isiyo ya aina yao,...tatizo kubwa ni kwamba mazingira yapo kinyume na kesho za watu wengi,hivyo kulipata somo hili na kuliishi,inahitaji ujasiri wa kutosha ,karibu tuendelee(tengeneza soko lako kabla ya safari)

ITAMBUE KESHO YAKO.
Hii ni hatua ya kwanza kabisa ya kuandaa kesho yako,bahati mbaya kwa upande wa Afrika ni watu wachache sana ambao wanafanikiwa kutambua kesho yao mapema,na wanaofanikwa kufanya hivyo ,wanashindwa kuifikia kwa kukusa maandalizi,kwa wenzetu wazungu ,hali ipo tofauti,wao hutambua kesho yao wakiwa na umri mdogo na wanaanza kutengeza mazingira mapema ya kuja kuiishi kesho yao..........Unafikiri kwa nini wao wanaweza?

Bill Gate akiwa na umri mdogo sana,aligundua kuwa anapenda sana kuchezea Computer,alichofanya alitafuta rafiki wa aina yake ambapo walitenga muda wa kuwa wanajifunza zaidi kuhusu computer kwenye Library ya shule,....akiwa na ndoto ya kumiliki company,alitumia muda mwingi kuwa kwenye mazingira yaliyomfanya awe mpya kila siku kwenye kile akipendacho,Je wewe hadi sasa hujagundua unapenda nini?,Je unakuwa mpya kila siku kwenye eneo lako?......Unafikiri tatizo ni  nini?


HALI YA KUSHANGAZA.

  • Watu wengi wanaifahamu mapema sana kesho yao,na wanajua kabisa jinsi ya kufanya ili waje kuishi kesho hiyo,ila tatizo ni uwezo wa kuthubutu unakuwa mdogo,...kama wewe unataka kesho umiliki kampuni,una maandalizi gani sasa?.....jaribu kutengeneza uhusiano wa kile unachokifanya sasa kiwe msaada wa kusaidia ndoto zako za kesho....kuna gharama,ila lazime uzilipe ili kuweza kuifikia kesho yako.

  • Watu wengi wa wengi tunakwepa maumivu kwa kuyahamishia kesho,....kuliko mtu kuanza maandalizi mapema ya kuandaa kesho ya malengo yake,anaona afanye maandalizi hayo kesho,unachokwepa leo nini?......kila siku ifanye iwe ya maandalizi ya kesho yako.

  • Watu wengi tunataka tuifikie kesho iliyo kamilika.....Hapa nakumbuka mwanafunzi mmoja aliwahi kuniambia,safari yake ya maisha itaanza baada ya kumaliza chuo,swali la haraka likanijia,....Atamaliza na umri gani?,kisha nikajiuliza,ina maana huyu mwanafunzi leo yupo anapoteza muda?,maana bado hajaanza safari ya maisha.
Kesho yako inaanza pale ambapo tayari umejitambua upo kwenye safari ya aina gani,kama safari yako inaenda kwenye kumiliki nyumba za kifahari,anza kuzitengeza leo,,,,,huwezi kuzipa ta nyumba hizo kwa siku moja,ujenzi wake unaanza leo,kila siku jitaahidi unapata maarifa ya kutosha kuhusu hizo myumba unazo zihitaji.



Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha,mkurugenzi wa label ya FIKIA NDOTO zako.

                    See You At The Top.
                        0652 134707

Friday, 13 October 2017

TENGENEZA SOKO KABLA YA SAFARI.

Karibu tena kwenye blog hii inayotoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa pumzi ambayo amekuwa akitupatia bure,karibu tujifunze.

KUSUDI LA SOMO.
Somo letu la leo linahusu umuhimu wa kutengeza soko kabla ya kuanza safari yoyote ya maisha,....Nafikiri wazo la haraka unaposikia neno soko ni biashara,lakini hapa nina maana zaidi ya soko la biashara,,,kabla ya kuendelea na somo jifunze kwanza somo hili (kwa nini hupigi hatua?).....karibu tuendelee.

MAANA YA NENO SOKO.
Kwa haraka ,soko ni sehemu ya kufanyia mauzo ya bidhaa/kitu flani,soko ni kipimo kizuri cha ubora wa kitu flani,mfano,soko la bidhaa flani likishuka,ni wazi kuwa ubora wa bidhaa hiyo unakuwa umeshuka.........Kwa maana pana zaidi na ambayo nataka ndio iwe sehemu kubwa ya somo letu ni hii,SOKO pia ni kipimo kizuri cha huduma yako,huduma yako inapimwa thamani sokoni,ubora wa huduma yako ndio unafanya soko lako liwe juu au chini.


KWANINI UTENGENEZE SOKO KABLA YA SAFARI?
Nafikiri umewahi kuona au kusikia majina ambayo yalifanya vizuri,ila hadi sasa hivi huyasikii tena,...tatizo ni nini?
Pia utakuwa umewahi kushuhudia mtu flani akianza kwa kasi kubwa na kwa ubora wa juu,ila baadae anapotea,tatizo ni nini?

Pamoja na sababu myingi zinazochangia hali hiyo,ila sababu nyingine kubwa ni watu wengi wanaanza safari bila ya kuandaa aina gani ya watu ambao watawafikia na changamoto zake,unapofahamu huduma yako itafikia watu wa aina gani (soko),itakusaidia uanze maandalizi ya kutosha kuhusu ubora wa huduma yako itayokidhi mahitaji ya watu hao kwenye vipindi tofauti tofauti .

Mazingira yanabadilika,mahitaji pia yana badilika,je umejipanga kuibadilisha huduma yako ili iweze kuendana na mabadiliko hayo?

Kabla ya safari ,hakikisha unatambua vizuri soko lako,tena utengeneze na soko mpya litalopatikana kulingana na mabadiliko yatayotokea,ukiendelea kutoa huduma ya aina moja muda wote,ubora wake utashuka kama ikitokea jamii imebadilika ila wewe hujabadilisha aina ya huduma yako.....TENGENEZA SOKO KABLA YA SAFARI.


Makala hii imeandikwa na Saul Kalivubha.
     mkurugenzi wa fikia ndoto zako label
       0652 134707.

Wednesday, 27 September 2017

KWA NINI HUPIGI HATUA?

Karibu tena kwenye blog hii  inayotoa elimu ya maisha na  jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa afya yangu ,ni matumaini yangu kuwa na wewe nimzima wa afya(sababu unapumua)..karibu tujifunze............

KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu hili ni kujifunza sababu ambazo zinazuia hatua za watu wengi,mimi pia ni moja ya wahanga wa sababu hizo,kwa muda mrefu nilikuwa nina mawazo makubwa ila sipigi hatua,na mwisho wa siku nayapoteza mawazo yale.....kwa nini hupigi hatua?


Kupiga hatua ni hali ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine,kutoka sehemu yenye viwango vidogo,kwenda kwenye sehemu  sehemu yemye viwango vikubwa zaidi,inaaweza kuwa kwenye biashara ,shule,urafiki ,uwekezaji n.k( jifunze elimu ya pesa)......Kuna watu wana mawazo mazuri,juhudi na wanajitahidi kujifunza kila siku ,ila bado hawapigi hatua mbele,bado matokeo wapatayo hayaendani na jinsi wanavyojituma........Tujifunze kupitia baadhi ya vikwazo vinavyozuia kupiga hatua kwetu.

 SABABU ZINAZO FANYA USIPIGE HATUA.

  •  Kuwa na imani kwamba kuna watu wanahitajika kukusaidia ili ufikie hatua flani,hii ni imani ambayo inasababisha watu wemgi wasipige hatua mbele kwa kusubiri aina flani ya watu waje watoe msaada,kwa lugha ya haraka tunasema connection au channels....sawa mafanikio yanahitaji watu,ila hata wewe unaweza kuwa channel kwa watu wengine kwa kujaribu kwako.Bahati ina nguvu kwa mtu mwenye juhudi,....jaribu hadi kwenye sehemu inayohitaji mtu wa kukusaidia,ili akitokea akute upo vizuri ki maandalizi

  • Usiogope makosa,....hapa ndipo kuna watu wenye mawazo mazuri sana na elimu ya kutosha kuhusu jambo flani,ila hawapigi hatua,..kwa nini? Watu wenye ujuzi mwingi mara nyingi hawtaki kuonekana wakikosea,bora waendelee kuwa na ujuzi wao kwenye fikra kuliko kujaribu kwa vitendo,hali hii ndio inafanya mara nyingi walimu kushindwa na wanafunzi wao...Hata uwe na elimu ya viwango vya juu kuhusu jambo flani,bila kuihamisha kwenye vitendo ni sawa na kazi bure,kubali kukosea ili upige hatua mbele kwa kufanya sahihi ,

  • Fanya maamuzi ,hata kama matokeo yake yanaumiza au yanapingwa na rafiki zako wa karibu,kuna watu tayari wanatambua ili kupiga hatua lazima wafanye jambo flani,ila kwa sababu tu jambo hilo linapingwa na marafiki ,wanaamua kuvumilia tu ili kuendeleza mahusiano mazuri ,Maisha ni ya kwako,rafiki wataokukimbia kwa maamuzi yako ya mafanikio ,achana nao,ukifanikwa watatafuta njia ya kutudi tena kwako

  • ,
  • Mafanikio ni haki ya kila mtu,hakuna aliyepangiwa viwango flani,hata wewe unawezakufika,ondo ile imani ya kwamba biashara flani inafanywa na watu flani tu,au ufaulu flani una watu wa aina flani tu,hata wewe umo kwenye watu hao ,,,,hivyo usiache malemgo flani kwa kuwa hakuna mtu wa familia yenu amewahi kufanya hivyo,,,,,,hutopiga hatua'

Makala hii imeandikwa na Saul kalivubha,kwa label ya fikia ndoto zako

Friday, 15 September 2017

SAIKOLOJIA YA PESA.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha ,nashukuru Mungu kwa kunipigania kwake kila siku, furaha yangu kubwa ni sababu  na wewe ni mzima.,kama ni mgonjwa pia ondoa hofu,yupo mponyaji mkuu kwa  ajili yako ambaye ni Mungu.

KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze saikolojia ya pesa katika sehemu kuu tatu ;BAJETI,AKIBA NA UWEKEZAJI....Kabla ya kuanza somo letu hili ni vizuri ukaelewa kwanza  maana ya Saikolojia kwa ufupi.
SAIKOLOJIA sio neno geni sana,ila kwa ufupi lina maana ya elimu ya tabia ,sababu zinazofanya utokeaji wa tabia na madhara ya tabia......kwa leo tujifunze tabia ambazo pesa inahitaji ili iweze kukaa mikononi kwako.......karibu tujifunze.



 BAJETI.
Bajeti ni muongozo ambao unahusisha mapato na matumizi ya pesa,ni watu wachache sana ambao wanatumia pesa kwa kufata bajeti,maana rahisi ni kwamba watu wengi hawana malemgo kwenye maisha yao ya kesho,haijalishi kipato chako ni cha ukubwa gani,lazima utengeneze bajeti ya kuonyesha pesa unayoingiza,matumizi unayotumia na akiba unayoweka.......Mambo muhimu sana ya kuzingatia kabla ya kupanga bajeti ni haya; Ukubwa wa pesa unayoingiza,  malengo yako yanayohitaji pesa ,  mazimgira yako(familia yako) na ufahamu matumizi ya lazima na yale yasiyo ya lazima....Mambo hayo machache yatakusaidia uishi maisha yanayo endana na bajeti yako ila yenye mchango mkubwa kwenye malengo yako ya kesho.



AKIBA.
Akiba ni pesa ambayo unahifdhi kabla ya kuanza matumizi yoyote ya pesa na kwa lengo maalumu,lazima uwe na malengo kisha ndio uanze kuweka akiba,Ukiona unashindwa kuweka akiba jitahidi upitie bajeti yako vizuri na kisha uanze kupunguza matumizi yasiyo ya lazima au kununua  vitu vyenye bei ya kawaida .....kiufupi lazima uishi maisha ya kawaida kwa sasa ili kesho uishi maisha ya tofauti,.....Kuna watu wanajidanganya kwmba kuweka akiba lazima uwe na kpato kikubwa,jibu ni hapana.....nakumbuka kuna kipindi nilikuwa naingiza laki moja kwa mwezi ila nilifanikiwa kupanga bajeti hadi kuweka akiba ya laki sita kwa mwaka,hivyo nikawa na jeuri ya kufanya kitu bora zaidiya kile cha kuingiza laki moja kwa mwezi.



UWEKEZAJI.
Ukiwa na bajeti nzuri utakuwa na uwezo wa kuweka akiba,usiweke akiba kama huna kitu cha kufanya kesho,utaitumia pesa yako ovyo,weka akiba kwa lengo flani,ili ile akiba ianze kukuzalishia pesa,......njia nzuri ya kutumia akiba ni kuwekeza au kufanyia biashara.....kwa hiyo ni vizuri kuwa na elimu ya pesa,elimu ya kile unachotaka kuwekeza na ukubali kuishi maisha ya kawida kwa muda flani.


            See you at the top
               Saul kalivubha
                  0652 134707

Sunday, 16 July 2017

SIRI YA KUMI YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nina imani wewe hapo ni mzima wa afya,kama ni mgonjwa usijali,Mungu yupo kwa ajili yetu wote.


  KUSUDI LA SOMO.
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya kumi ya urafiki ambayo ni UKWELI ,ila kabla ya kuendelea mbele ni vyema ukapitia na kujifunza kwanza siri ya tisa ya urafiki(SIRI YA TISA YA URAFIKI).


           SIRI YA KUMI  YA URAFIKI   (UKWELI).
Kwenye urafiki kuna kuwekana wazi mambo,ila kabla ya kuweka wazi mambo yako kwa rafiki yako lazima kwanza uwe umejihakikishia uaminifu wa kutosha ,ila wakati mwingine kuna watu wapo kwenye urafiki kwa kuficha ukweli,wanatumia uongo kutengeneza ukaribu wao....je hii ni sahihi?


Wanasaikolojia wa mambo ya mahusiano wanazungumza kwamba ...Watu wanatafuta wasiyoyafahamu,hawana shida na wanayoyafahamu,,,hii tafasiri yake ni kwamba rafiki yako anatafuta mambo ambayo hayafahamu kutoka kwako,inaweza kuwa umemdanganya jambo fulani,siku akilifahamu lazima sura ya urafiki wenu ubadilike,...jifunze kuwa mkweli.


Ni bora kumficha mtu jambo kuliko kumdanganya,sababu za kumficha mtu jambo zinaweza kuwa zina maana kubwa kuliko sababu za kumdanganya mtu,,,,,kumdanganya maana yake umemwambia ukweli wenye hila ndani yake,umetafuta kuaminiwa kwa njia isiyosahihi.



Ukiona rafiki yako amekukwepa kwa sababu umemwambia ukweli,jua huyo sio mtu mzuri kwako,maana ukweli una thamani kubwa sana kwenye urafiki wa kweli,urafiki ambao una lengo la kufikia mafanikio makubwa.


Tatuzo ukisha anza na uongo tu kwenye urafiki wako,itakufanya kila siku uendelee kutengeneza uongo wa kudumisha uomgo wa mwanzo....urafiki wa aina hiyo una umuhimu gani?, ukijiona mjanja wa kudanganya ,tambua thamani yako inashuka,pia unapoteza muda wako kudanganya na kuendeleza uongo wako.



Kitabu cha SIRI ZA URAFIKI kinaelekea kuwa tayari,utakipata kwa mawakala wa fikia ndoto zako....


                           See you at the top.
                    Scientist Saul kalivubha.
                              0652 134707

Monday, 10 July 2017

SIRI YA TISA YA URAFIKI

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa mafunzo ya maisha na jinsi ya kufikia ndoto zetu,nashukuru Mungu kwa uzimab wake kwangu ,pia ni imani yangu kuwa wewe ni mzima........karibu.



   KUSUDI LA SOMO.

Tunaendelea na somo letu la siri za urafiki,leo ni siri ya tisa ambayo ni mipaka ya ufahamu,...kabla yakuendelea na somo letu hili,ni vyema ukajifunza kwanza siri ya nane ya urafiki(SIRI YA NANE).,karibu tuendelee.



SIRI YA TISA YA URAFIKI(MIPAKA YA UFAHAMU).

Katika urafiki ni jambo la kawaida sana kufahamu habari za rafiki yako,swala hili ni zuri sana ikiwa unataka kufahamu habari hizo kwa lengo la kudumisha urafiki,ila kuna habari zingine za rafiki yako zinaumiza,kama hauna ujasiri,badala ya urafiki kuimarika,utavunjika......kabla ya kuanza kuzifatilia habari za rafiki yako jitahidi kufahamu haya.

  • Weka mipaka,hakikisha unafahamu mambo yenye fada tu katika ujenzi wa urafiki.
  • Kuwa makini na chanzo cha habari, sio kila chanzo cha taarifa za rafiki yako ni chanzo sahihi.
  • usifatilie habari za rafiki kama kumpeleleza,akijua urafiki wenu utapoteza uaminifu,kuwa mpole na taratibu tu utafahamu mengi kuhusu yeye.
  • Fanyia kazi mambo utayo yafahamu kwa rafiki yako kwa lengo la ujenzi na sio kwa leng la kumuhukumu rafiki yako.


Mwamdishi mmoja wa mambo ya saikolojia aliwahi kuandika kanuni moja muhimu sana ,kanuni hiyo ni hii   "Msongo wa mawazo(Stress) unaongezeka,kila ufahamu unapoongezeka"
Kanuni hii inasaidia kupunguza kufahamu mambo yasiyokuhusu,watu wengi kwenye urafiki wanaishi kwa mawazo kwa sababu tu walifatilia mambo yasiyo wahusu ya rafiki zao.


Kuna mambo sio lazima uyafahamu kutoka kwa rafiki yako,utaumiza kichwa bure tu,tena kibaya zaidi hakuna uwezo wa kuyabadilisha mambo hayo,tena kuyafahamu kwako hakuna faida yoyote kwenye uraki wako .....


                        See you at the top.
                            Saul kalivubha
                               0652 134707.

Sunday, 2 July 2017

SIRI YA NANE YA URAFIKI.

Karibu tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya mafunzo ya maisha, nashukuru Mungu kwa uzima wangu na wako pia. ......Karibu sana kwenye muendelezo wa somo letu la urafiki, nina imani kuna kitu unajifunza. ..karibu.

LENGO LA SOMO. 
Lengo la somo letu la leo ni kujifunza siri ya nane ya urafiki kulingana na mpangilio wangu, siri hiyo ni  Jichunguze tabia yako. ... .Unaweza pitia kwanza SIRI YA SABA, kisha uje tuwe wote. .....karibu tuendelee.

SIRI YA NANE  (JICHUNGUZE TABIA YAKO ).

Urafiki unapitia mazingira mengi sana, kila mazingira huwa yanahitaji style  (mfumo ) wa kuishi ili kuhakikisha urafiki unaendelea na thamani yake.Ila kuna kipindi mtu anaona rafiki yake kabadilika tabia, amekuwa na tabia mpya ambayo hapo nyuma hakuwa nayo.

  • Je umewahi kukutwa na hali hiyo? 
  • Urafiki wako ulikuwa na sura gani baada ya hali hiyo? 
  • Unafikiri chanzo chake ni nini? 
Ni hali ya kawaida sana kusikia mtu akilaumu kuhusu kubadilika kwa tabia ya rafiki yake, tena kwa sababu nyingi za kujiona yeye mshindi na kumfanya rafiki yake kuwa mwenye hatia. ..
Tabia inatoka wapi?
Kila tabia lazima itanguliwe na mazingira flani, mazingira ambayo ndio chanzo cha tabia hiyo, hakuna tabia inayo tokea bila kusababishwa. ....!
Inawezekana tabia ya rafiki yako imetokana na mazingira yako, mazingira uliyoyajenga kwa huyo rafiki yako. Hakikisha kabla ya maamuzi ya kumpoteza rafiki yako kwa kigezo cha kuwa na tabia mpya,Jichunguze kwanza wewe, Jichunguze tabia yako, inawezekana wewe ndio chanzo.

Kumpoteza rafiki zako bila kujifanyia uchunguzi kwanza, ni kosa kubwa sana, unaweza usidumu na rafiki yoyote kwa sababu tu hujafanya mabadiliko ya tabia yako. .
Tukutane wiki ijayo.

            See you at the top.
           scientist Saul kalivubha.
               0652 134 707.
0