Thursday, 26 January 2017

NDOTO YA MSIMU -1

Nakukaribisha tena kwenye blog hii yenye kutoa elimu ya maisha,binafsi namshukuru Mungu kwa makuu yake kwangu, nina imani na wewe ni mzima.
Bado tupo mwanzo wa safari, kila anaye jitambua najua yupo makini na aendapo.

.
   KUSUDI LA SOMO.
Leo nataka tujifunze somo la,NDOTO YA MSIMU,   katika somo hili tutajifunza mambo makuu matatu.
1.MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
2.CHANZO CHA MTU KUWA NA NDOTO YA MSIMU.
3. MADHARA YA NDOTO YA MSIMU.

    1.MAANA YA NDOTO YA MSIMU.
Ndoto, ni jumla ya picha mtu anayokuwa nayo kuhusu kesho yake, watu wengi huchanganya kati ya "ndoto"  na "malengo "
Malengo ni sehemu  ndogo ndogo ambazo mtu anapaswa kuziunganisha ili kuifikia ndoto yake.

Ndoto ya msimu ni picha ya maisha ambayo mtu huichora kwa kuchochewa na mabadiliko ya mazingira(msimu ).
NB. ....Ndoto ya msimu inaweza kubadilika na kuwa ndoto ya kudumu ila ni watu wachache sana ambao wanafurahia maisha yameyojengwa na badiliko hilo. ...wengi hujuta.

Kwa upana wa kulielewa vizuri somo hili, pitia mifano hii michache.

#  Wanafunzi wengi katika levels zote za elimu huwa wanajikuta wanatengeza ndoto zao kulingana matukio yanayofanyika shuleni,  ila baada ya siku chache kupita baada ya tukio kuisha, wanafunzi hao husahau kabisa kuwa waliweka ndoto flani. ..siku mazingira ya tukio yakijirudia ndipo wanafunzi hao hupata kumbukumbu (ndoto ya msimu hiyo ).

#Watu wengi mwishoni mwa mwaka huwa wanatengeza ndoto nyingi ili mwaka mpya waweze kuzikamilsha. ....ila mambo huwa tofauti, mwaka Ukianza mpya wanasahau kuwa kuna mambo walijiwekea kuyafanya.
Hali hiyo kuna uwezekano ikawa inasababishwa na mada kuu inayo zungumzwa mwishoni mwa mwaka. .....mwishoni mwa mwaka neno MALENGO huwa kwa wingi masikioni kwa watu, hivyo mazingira hayo humfanya mtu kutengeneza ndoto nje ya uhalisia.

#MAHUSIANO, kuna mtu humpenda mtu kulingana na mazingira, mtu huyu hujikuta moyoni mwake  anatengeneza picha juu ya mtu yule kuhusu kesho yake. ....hatari zaidi mtu huyo kulingana na uchochezi wa mazingira hujikuta anafanya AGANO la kudumu kwenye Upendo wa msimu. .....siku mazingira yale yakipotea mtu huyu ndipo anagundua yupo sehemu isiyo sahihi(ndoto ya msimu )

Nina imani kwa mifano hiyo somo limeeleweka kwa kiasi flanI.
Jiulize ,ndoto uliyonayo ni ya msimu? Kama ndio, umewahi kufikiria ni hali gani utakuwa nayo siku mazingira yameyotengeneza ndoto yako yakitoweka?
NB. ..
Kabla ya kuchukua maamuzi hakikisha umefahamu madhara ya ndoto ya msimu.



                                       See you at the top.
                                       Scientist Saul Kalivubha.
                                              0652 134707.. 

Friday, 20 January 2017

JITAMBUE 2

Nimshukuru  Mungu kwa siku nyingine hii, pia niseme asante kwake kwa uzima wako, Karibu tena kwenye blog hii kwa series ya somo letu la KUJITAMBUA.
Week iliyopita tulijifunza SIFA ZA MTU ASIYE JITAMBUA. ......kama hukupitia somo hilo ni vyema ukalipitia kabla ya kuendelea na hili la leo  (http://kalivubha.blogspot.com/2017/01/jitambue.html?m=1).

Leo nataka tujifunze sehemu zilizobaki kwenye somo letu hili. .....nazo ni MADHARA YA KUTOJITAMBUA NA JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA KUTOJITAMBUA. ..


        2.MADHARA YA KUTOJITAMBUA.
Kutojitambua ni tatizo ambalo  limefanya wahusika wawe sehemu zisizo sahihi  (kwenye mahusiano, biashara, mafanikio n.k).
Madhara ya kutojitambua ni matokeo ya kuwa sehemu isiyo ya kwako. ......

 Madhara makubwa ambayo yanaweza beba yote kwa mtu asiye jitambua ni kutofanikiwa kwa jambo lolote, huwezi fanikiwa ikiwa hujui wapi umetoka, wapi ulipo na wapi uendapo, ili mtu afanikiwe kwa jambo lolote lazima ajue vizuri sehemu anayoenda, ikiwa haitoshi lazima mtu atambue vizuri mazingira ya kumfikisha aendapo.

Mtu asiye jitambua mara nyingi hushangiliwa na watu wavivu(watu wanaopenda sehemu rahisi )  hii humfanya mtu huyo kuendelea kufanya mambo ambayo yapo kinyume na jamii inayojitambua, hivyo mtu huyu hupoteza uaminifu. ....

  3. JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA KUTOJITAMBUA.  
Kutojitambua huwa nasema ni ugonjwa kwa sababu kila mtu anaweza ambukizwa tabia ya kutojitambua kutoka kwenye mazingira.
Huwa ni rahisi kuzuia ugonjwa huu, ila ni Kazi kubwa sana kuutibu endapo mtu akiupata. ...hii hutokana na wagonjwa wa tabia hii kuwa wagumu kukubali kuwa ni victims.

 Ili mtu apone ugonjwa huu inabidi kwanza yeye mwenyewe atambue kuwa ni mgonjwa, kisha hatua inayofata ni zoezi la kubadili MARAFIKI. .....maana mtu asiye jitambua kuna uwezekano mkubwa hata rafiki zake hawajitambui pia.
Zoezi la kubadili rafiki huwa ni ngumu kidogo  (lina hitaji ujasiri ) Ila ndio tiba pekee ya kuaminika kwa mgonjwa wa aina hii.


Let's meet on the next week , we will be having  a new lesson termed as NDOTO YA MSIMU.



                    see you at the top
                    Scientist Saul kalivubha.

Thursday, 12 January 2017

JITAMBUE 1

 Nashukuru Mungu kwa uzima wangu, bila shaka wewe pia ni mzima wa afya. Ni utamaduni mzuri sana kuwa na ibada ya kumshukuru Mungu kwa makuu yake.

KUSUDI LASOMO
.Tukiwa bado tupo kwenye safari ya maisha nimeona vyema tujifunze somo la KUJITAMBUA. Somo hili litakuwa na sehemu tatu.

   1.SIFA ZA MTU ASIYE JITAMBUA.

  2.MADHARA YA KUTOJITAMBUA.
                        3.JINSI YA KUTIBU UGONJWA WA KUTOJITAMBUA.


Kujitambua kwa maana (definition) rahisi ni kufahamu vizuri mazingira yako, ..kufahamu mazingira yako tu haitoshi, kufahamu kwa nini upo kwenye mazingira hayo ndo Kujitambua kamili.
Kuna uwezekano kuwa watu wengi wapo maeneo yasiyo sahihi kwa sababu tu hawajitambui, na wataendelea kuwa maeneo hayo sababu  ya tatizo la kutofanya TASMINI.


                         SIFA ZA MTU ASIYE JITAMBUA

Kutojitambua
ni tatizo ambalo wengi wetu tunalo,ila ukiwa hujakutana na mazingira ya kulichochea tatizo hilo ni vigumu kuona dalili zake. ......na mara nyingi mtu mwenye tatizo hilo huwa hakubali kama analo. ....

zifatazo ni baadhi ya sifa za mtu aliye na tatizo la KUTOJITAMBUA.

KUTOKUWA NA MALENGO : hii inaweza kuwa ni sifa kuu ya mtu asiye jitambua,  neno malengo kwake anakuwa analisika tu. Kumbuka tu usipokuwa na malengo huwezi kujua usahihi wa eneo ulilopo, kila jambo kwako utaona sahihi ila mazingira yakibadilika kidogo utaona sio eneo sahihi kwako.

 KUTOKUWA NA RATIBA; mtu asiye jitambua huishi kwa ratiba za watu wengine,  kama huna ratiba ya kuongoza maisha yako ni ngumu  kuwa na mipaka ya kulinda muda wako. .....kila ratiba ya nje itakuwa inafanya mabadiliko kwako...kumbuka tu watu hupenda sehemu rahisi, kila wakiwa na free time hutafuta sehemu rahisi ya kupumzikia. ...mtu asiye jitambua huwa busy kwenye free za watu wengine.


KUWA TAYARI KUACHIA ALICHO NACHO; ..Ni jambo jema mtu kufanya tasmini na kubadili mazingira  (endapo akigundua hayupo sehemu sahihi ,ila hii ni tofauti kwa mtu asiye jitambua, ..mtu huyu yupo tayari kuacha sehemu salama na kuelekea pasipo salama,  hii mara nyingi hutokana na tabia kutojiamini (tabia ya mtu asiye jitambua ).....ni vigumu kuamini kitu ulicho nacho na wakati hujui sahihi ni kipi, na ukikosa imani na ulicho nacho just muda wote utakuwa na mawazo ya kukiacha.


KUISHI KWA MAZOEA;  mtu asiye jitambua huishi kwa mazoea, muda wote yeye anakuwa anaamini kufanya mafanikio mwisho wa safari yake,  kwa kuwa amepoteza kujitambua,mtu huyu
hana sababu za kwanini yupo  pale alipo. ....swali zuri la kujiuliza siku zote ni " upo hapo ulipo kwa sababu wengine wapo or upo kwa sababu lipo kusudi la wewe kuwepo hapo ?"


KUKOSA UVUMILIVU; mtu asiye jitambua hana uvumilivu hata kidogo, hii hutokana na kutojua  umuhimu au hasara wa alicho nacho, ni vigumu kuvumilia na huku hujui kwa nini unavumilia. ......wavumilivu ni wale wanao tambua mazingira yao vizuri.


      KUTOJITAMBUA ni ugonjwa wa kuzuia mafanikio, ugonjwa huu tafasiri yake ni sawa na msafiri ambaye huchukua maamuzi ya kupanda gari bila kujua aendapo.

.......welcome again next session on next week.

                 See you at the top.
             Scientist Saul kalivubha.
                 0652 134707


Thursday, 5 January 2017

MAAMUZI

Nimshukuru kwa kunipigania kila siku, hadi sasa nipo salama. .....ni vyema kama na wewe una utaratibu wa kumshukutu Mungu.....

KUSUDI LA SOMO. 

Leo nataka  tujifunze machache kuhusu  Maamuzi......karibu tujifunze,

                  MAAMUZI. .....

 Mwandishi :Saul kalivubha.

Maamuzi kwa mtazamo wangu huwa nasema. ....Maamuzi ni miguu,  usipofanya maamuzi huwezi piga hatua. ..
Mazingira tunayoishi yamebeba mambo mengi,...ili kupiga hatua lazima tuchague machache kati ya mengi. ...maamuzi ni kuchagua pia na ni changamoto kubwa sana kwenye mafanikio yetu. ...

                  MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU MAAMUZI. 
Unapofanya maamuzi, fahamu kuna hatua itafata ambayo ni utekelezaji, kabla ya utekelezaji  ni bora ukatasmini upya maamuzi yako. hii nafaida kubwa, maana mara nyingi mtu hufanya maamuzi kulingana na hali aliyonayo muda huo. .....inawezekana maamuzi yako sio halisi ila ya hali uliyokuwa nayo tu. ....je hali hiyo ikitoweka bado utaona upo kwenye maamuzi sahihi? 

Sifa kubwa ya maamuzi sahihi ni kuwa na matokeo yenye changamoto, Hapa ndipo wengi hujikuta wakibadilisha msimamo. ....Maamuzi sahihi ni chukizo kubwa kwa rafiki zako wanaotamani usitembee, changamoto zitaanzia kwa wao kupinga utekelezaji wa maamuzi yako. Kwa sababu wengi wetu hufanya maamuzi ili kufurahisha watu, tukiona rafiki zetu huchukia maamuzi yetu na sisi hubadili msimamo wetu. ......usiogope kupoteza rafiki walio kinyume na wewe,kumbuka tu bila maamuzi huwezi kupiga hatua. 

Kama una ugonjwa wa kukata tamaa hakikisha unafanya maamuzi ya kutibu ugonjwa huo kabla ya kufanya maamuzi mengine. ....almost watu wote waliokata tamaa huwa maamuzi yao ni sahihi kwao ila huwa hayana mafanikio. ......mtu aliyekata tamaa huwa na imani flani akilini mwake, hivyo imani yake ndio hutwala maamuzi yake.Imani ya mtu aliyekata tamaa ni  ni HOFU. .....ukifanya maamuzi ukiwa na hali ya hofu jiandae kupokea matokeo yenye kukatisha tamaa zaidi ya mwanzo. 


Ukishindwa kufanya maamuzi, mazingira yatafakufanyia maamuzi. ....wapo watu ambao hawajui waendapo wala watokapo. ..ni vigumu kusema jambo hili sio sahihi na huku sahihi hulijui,hivyo ukiwa kwenye hali hiyo tayari umetoa kibali cha mazingira kukufanyia maamuzi. 
Tatizo hili wanalo wengi, ili ujue kama una tatizo hilo jaribu kutasmini maamuzi unayofanya ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu. .....jiulize hayo maamuzi ni yako au ni influence za wanaokuzunguka? ............


Watu ambao mazingira yamewafanyia maamuzi ila bado wanahisi ni maamuzi yao kuna uwezekano kuwa hawapo sehemu sahihi  (iwe  kwenye mahusiano, ndoa, biashara nk).
Jitahidi uwe makini kwenye maamuzi. 


                             See you at the top.
                      scientist Saul kalivubha.
                                  0652 134707.


Saturday, 31 December 2016

ANZA KWA MAFANIKIO

Nawasalimu nikiwa nimejaa nguvu ya Mungu wetu,nina imani nyie wote ni wazima.  Moja ya vitu ambavyo wengi wetu tunatamani, ni ujuzi wa kuanza safari ili tufike salama. Leo nataka tujifunze machache ambayo yanaweza kukusaidia kuanza mwaka wako vizuri.
Mwisho mazuri, sometimes hutegemea mwanzo mzuri pia. Unaweza anza safari yako kwa kufanya hayo :

                                     WEKA MALENGO
Andika ambayo unatarajia uyafikie ndani ya muda umeojipangia, kupanga malengo sio Kazi rahisi, hakikisha mazingira ya nje hayawi kivutio cha wewe kuweka malengo, usiweke malengo sababu upo kwenye kundi ambalo ili uendano nalo lazima utimize kama walivyo wao. Jitahidi sana kesho yako iwe na asilimia nyingi za maamuzi yako.


                                        TENGENEZA MAZINGIRA KULINGANA NA MALENGO YAKO.
Kuweka malengo sahihi ni wachache wanaweza fanya, kuishi katika mazingira yenye kubeba malengo inawezekana ni 1 ya 10 wanaoweza fanya. Tambua kila malengo yana mazingira yake,huwezi kusema una malengo kuibadilisha kesho yako ikiwa rafiki tu wa karibu haijui kesho yake. ........kuishi katika mazingira yenye malengo yako ni kutangaza vita na walio kinyume na wewe. .........ndo mana sio zoezi rahisi, linahitaj ujasiri.

                                  TENGENEZA MIPAKA
Huwezi fanikiwa kama huna mipaka ambayo watu wanaifahamu.....mipaka nina maanisha uwezo wa kutoingiliwa zaidi ya kawaida. .......usipokuwa na mipaka, huwezi control ratiba zako,utakuwa unafanya ratiba za wengine, wengi watakupenda kwa urahisi wako ila mwisho wa siku utapata ugonjwa wa kulizika na kisicho sahihi.

                                        AMUA KUENDELEA.
Unaweza timiza yote hapo juu ila usifanikishe malengo yako,  huwezi kutimiza malengo yako endapo hujaamua kuendelea, kuamua kuendelea ni kuanza kufata hatua za kutimiza malengo yako. .........ukihitaji ufaulu mzuri lazima uamue kusoma kwa juhudi.

                          TASMINI MALENGO YAKO.
Swali zuri kwa mwenye malengo ya kweli ni hili. ......"kwa nini nimeweka malengo haya? "
Kuna sababu nyingi zinazofanya watu waweke malengo yao, ila sio kila sababu iliyokusukuma ipo sahihi, ni vyema kama utakuwa na muda mzuri wa kuhakiki malengo yako.


NB: Wanaofanikiwa mara nyingi ni wale wenye sifa ya uvumilivu na wenye rafiki wa kweli.
        Swali zuri jiulize. .....rafiki yako yupo tayari kuwa na wewe kwa Upendo ulele endapo utamtangulia kufanikiwa?

See you at the top
Scientist Saul kalivubha
Tembelea blog hii jumatano na jumapili kwa masomo mapya.


     

Tuesday, 27 December 2016

SIFA ZA MTU ALIYEKATA TAMAA

Nashukuru Mungu kwa uwepo wake kwangu, anazidi kuonekana katika maisha yangu. Imani yangu ni kuwa wewe pia Mungu anaonekana kwako . Tukiwa mwishoni mwa mwaka huu,, nataka tujifunze machache kuhusu mtu aliyekata tamaa.                                                                        Muhimu ni kuwa huwezi fanikiwa ukiwa umekata tamaa.  Hapa chini ni baadhi ya sifa za mtu aliye kata tamaa.
1 . Huwa anakuwa na sababu nyingi za kutetea hali aliyonayo, kwenye ufahamu wake anakuwa na mifano mingi ya walioshindwa tu. 

2 . huwa anaamini mafanikio ni bahati na sio juhudi, kila aliyefanikiwa kwake humuona mwenye bahati na haamini kuwa juhudi zina nguvu katika mafanikio. 

3. Hapendi mafanikio ya wenzake, na hii ndio sababu yeye pia hafanikiwi. .....huwezi fanikiwa ukiwa hupendi mafanikio ya wenzako. 

4.huwa ni mtu wa kulaumu muda wote, hutafuta uadui na wanaomshinda....muda mwingi huwatafutia sababu waliofanikiwa  zaidi yake. 

5. Rafiki zake pia ni wenye sifa za kukata tamaa, ndio mana huwa ni ngumu kwa mtu aliyekata tamaa kubadilika. .....maana huwezi kuwa na mawazo tofauti na rafiki zako. .na ukifanikisha kuwa na mawazo tofauti huwezi kuwa na rafiki ambao mmepishana. 

6.mtu aliyekata tamaa  huwa anajaribu kutafuta short cut za kufanikiwa......siku zote kufanikiwa kwa ujanja ujanja mwisho wake ni kufa maskini. 

NOTE :Kukata tamaa ni ugonjwa, ugonjwa huu mara nyingi hutokana na historia ya mtu aliyopitia. ....inaweza kuwa ni kwenye mahusiano,biashara, Masomo etc 
             
           Huwa sio Kazi rahisi kutibu ugonjwa huu kwa haraka, kumbe ukiwa na rafiki mwenye kukata tamaa jitahidi maisha yako yawe sehemu ya  kumbadilisha(ingawa ni hatari sana kuwa karibu na aliye kata tamaa, badala ya kumbadilisha unaweza badilika wewe )

Jitahidi sana uwe makini na historia umeyopitia, uliyopitia jana, juzi au miaka ya nyuma hayana mahusiano na mafanikio yako. ......ila kama ulifanya maamuzi ya kudumu kwa uliyopitia ,tayari utakuwa umeingia tayari kwenye kundi la watu walio kata tamaa.
                See you at the top.
              scientist Saul kalivubha.
                       0652 134 707. 

Friday, 23 December 2016

MWISHO WAKO, MAFANIKIO YAKO

Ni tumaini langu kuwa wote ni wazima wa afya, tukiwa mwishoni mwa mwaka huu najua kila mmoja mwenye Upendo na kesho yake yupo busy na tasmini ya safari yake ya maisha. Kumbuka kumshukutu Mungu kwa viwango umevyofikia, haijalishi ni kwa hatua gani umefikia malengo yako

Leo kuna vitu vitatu vitatu nahitaji tujifunze kuhusu mahusiano ya mafanikio na maamuzi yetu tuyafanyao tukiwa kileleni mwa safari,
Hapa ndipo wengi tunakosea na kuharibu uzuri wa hatua zetu za nyuma, yafatayo ni mambo ambayo wengi wetu huyafanya tukiwa kweny kilele cha  safari

KULEWA NA MAFANIKIO :   ili kuhamia upande wa pili ni vyema ufanye tasmini ya upande wa kwanza ili ujue jinsi ya kuanza upande wa pili. .tasmini ikionyesha mafanikio huwa kuna changamoto kwa anayepokea mafanikio hayo,   usipokuwa kuwa makini utajikuta unaishi maisha ambayo yamebebwa na ziada uliyoipata na sio uhalisia wako, Hapa ndipo wengi tunajikuta tunanua mambo yenye kupunguza tamaa za miili yetu na kusahau kuwa kufanikiwa sio mwisho wa kutafuta.

KUKATA TAMAA :tasmini yako ikionyesha kushindwa huwa ni changamoto kwa mtu muhusika, wengi hapa hujikuta hufanya maamuzi ya kudumu kwa hali ya muda mfupi, mfano mtu ambaye alikuwa na lengo la kufunga ndoa mwanzoni mwa 2017 lakin mwishoni mwa mwaka 2016 anaachana na mchumba wake. ..kweny mfano huu wengi huwa wanafanya maamuzi ya kudumu na kujikuta anapteza imani ya watu wote wa aina ya aliyeachana nae. Yapo maamuzi meng ya kudumu tunayafanya mwishoni mwa tasmini na kuishi maisha yenye matendo ya maamuzi hayo huku tukisahau kuwa hali ya muda mfupi huwa ni changamoto na sio tatizo.

KUFANYA AGANO :kuna philosophy inasema " epuka kufanya AGANO na mtu ukiwa ktk furaha au huzuni"......tasmini yako ya mwaka ina matokeo ya aina mbili , mafanikio au kuwa chini ya mafanikio, je hali hiyo imekufanya uweke AGANO na mtu?  hakikisha umejipa muda wa kutosha baada ya tasmini yako kisha uwe huru kufanya AGANO na watu  (rafiki ).



Nikutakie maandaliz mema ya Christmas.
Scientific Saul kalivubha, see you next session!